|
ZAHRAU
|
ZAHRAU NI WAAMINIFU
Mudiir wa taasisi ya kiislamlu ya Zahrau ya jijini Tanga sheikh Mohammed Suleiman amesema taasisi ya Zahrau ni ya waaminifu hivyo yeyote mwenye haja ya kuchangia maendeleo ya waislamu afanye hivyo kupitia kwao bila kuwa na shaka yoyote.
Tamko hilo alilitoa katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Zahrau (Zahrau Day) yanayofanyika kila mwaka katika makao yake makuu hapo Msambweni Tanga.Sherehe za mwaka huu zimefanyika kwa siku 3 kuanzia mwezi 10 shaaban 1431 mpaka mwezi 12. Wageni mbali mbali walipata fursa kutoa nasaha zao kabla ya kuhitimishwa mnamo usiku wa manane.
Akikariri tamko lake la uaminifu, sheikh Mohammed aliorodhesha jumla ya miradi ambayo imegharimu mamilioni ya fedha kutokana na michango midogo midogo ya waislamu na kutumika kama ilivyokusudiwa.Jengo ambalo limekamilika ni bweni la wanafunzi ambalo mpaka kukamilika kwake limegharimu shilingi milioni mia tatu (300,000,000/=).Mradi mwengine alioutaja ambao tayari umeanza ni ujenzi wa jengo kwa ajili ya mayatima, ambalo nalo linatarajiwa kutumia shilingi milioni 260 mpaka kukamilika kwake.
Sheikh Mohammed alilazimika kutangulizwaa nasaha zake kutokana na majukumu ya kiofisi yaliyokuwa yakimkabili usiku huo.Kwa mujibu wa mkuu wa itifaki wa hafla hiyo, mudiir wa Zahrau mara kwa mara hufuatwa kwa mashauri mbali mbali ya kiserikali.Usiku huo alitakiwa akamilishe suala fulani ambalo lilitakiwa liwe limefika Dar es salaam mapema siku inayofuata.
Katika moja ya maonesho ya kielimu ya wanafunzi chini ya taasisi hii,kijana kutoka Kondoa alieleza umuhimu wa malezi kwa vijana wa kiislamu.Aliposimama kusherehesha onesho hili, sheikh Mnyamisi alisema malezi ya vijana wa kiislamu ni lazima yaendeshwe na waislamu wenyewe.Haiwezekani kwa watoto wa kiislamu kulelewa kwenye shule za awali za makanisa, yaani kusimamiwa malezi ili wapate mafanikio katika dunia na akhera zao.Kufafanua hili alisoma aya ya 141 ya surat Nisaa (4:141) inayosomeka …Na Mwenyezi Mungu hatawajaalia makafiri njia ya kuwashinda waislamu.
|
| |
|
GAYS SEMINAR
|
The planned visit and seminar by gays community is likely to cause chaos in Tanzania.For second straight week, this issue has been the sermon topic during Friday prayers at several Tanga city mosques.
Sheikh Muhsin Ame during last week’s prayer warned muslims not to live in a house which one of its occupants is a known gay or lesbian.He said this on a podium in front of a full packed Boraska mosque situated at Raskazone area.Normaly this mosque attracts worshipers from far away in the city.
The same topic was repeated today; 2nd July 2010 in a harsher tone by sheikh Abdallah Chembeye who is a tutor at Ma’ahad imam Shaafiy situated at Sahare,the coastal ward in the city.He presented his sermon during the Friday prayer conducted at masjid Hanafi in the city center,close to Hindumandal dispensary and behind Tigo cell phone company office for Tanga region.
He reiterated the warning by saying that If the government of Tanzania does not stop this visit and seminar,then to get prepared to the wrath from Allah which unfolds in various forms.
Sheikh Abdullah said, while the most prefered punishement to gays and lesbian participators is killing them,the imams of the four schools of thought have got different opinions on how to execute the punishment.He said,the immediate followers of Prophet Muhammad,peace be upon him ,suggested various methods deriving their arguments from the Qur’an and sunnah.
Some of the prophet words concerning gays in Kiswahili, mentioned during the prayer are “Ye yote mtakayemkuta akitenda tendo la kaumu Luti (liwati), basi waueni mtendaji na mtendwa”. Abu Daawoud, Ibn Maajah & Tirmidhiy, “Mrujumuni wa juu (mtenda) na yule wa chini (mtendwa)”. Ibn Maajah. “Amelaaniwa mwenye kutenda matendo ya kaumu Luti”.
Ibnu Abbas says such offenders have to be taken to a particular areas tallest building and dropped head down,upon touching the ground to be followed with stone hits from a crowd until He/She dies.This is derived from Allah’s punishement to Qaumu Lutt as mentioned in Qur’an 11:82-83.According to these verses Allah,the almighty ordered His Angel;Jibril to pick up the village of qaumu Lut and then drop it upside down, where by later Allah sent rain and pelted the land with hot stones from jahannam.This is among severest punishements by Allah to mankind,showing how disgusting the gays and lesbian activities are to Him.
The same preacher after the khutba lead the congregation prayer reading Qur’an from surat Hud from which the Qaumu Lut is mentioned. Several worshipers could be heard weeping silently.
According to reports by several news medias,the gays and Lesbian communities from all over the world have planned to run a seminar at the University of Dar-es-salaam from July 19 up to August 6 ,2010. The organiser of that seminar is APSA-American political science Association. Before switching to Dar es salaam,it was planned to be held in Uganda but people there protested heavily to the idea.
|
| |
|
KUFRU YAVUNJA AMANI
|
KUFRU CHANZO CHA KUVUNJIKA AMANI Imeelezwa kuwa kufru hasa ya ushirikina ni chanzo kikuu cha kuvunjika kwa amani katika nchi.Hayo yameelezwa na mufti wa Tanzania,sheikh Issa Shaaban Simba mara baada ya swala ya Ijumaa katika msikiti wa Boraska uliopo eneo la Raskazone jijini Tanga.mwishoni mwa mwezi wa Jamadul aakhir sawa na tarehe 11 juni 2010.
Hizo zilikuwa ni nasaha zake wakati alipopewa nafasi ya kusalimiana na waislamu akiwa njiani kuelekea mji wa Mombasa nchini Kenya.
Alitahadharisha uwezekano wa kuvunjika kwa amani katika kipindi cha uchaguzi mkuu wa kidemokrasia unaoikabili Tanzania mwaka huu.Alitoa wito kwa waislamu kujitokeza kuwania nafasi mbali mbali za uongozi katika uchaguzi ujao ili huenda kuwepo kwao katika nafasi hizo wakatoa dokezo zinazoweza kuwa nusra kwa waislamu na kwa nchi kwa jumla..
Mada ya amani ilikuwa ni sehemu ya khutba ya Ijumaa iliyotolewa na sheikh Hashim Rusaganya mapema katika msikti huo.Katika kuifafanua aya ya 112 ya surat Nahl,alisema ushirikina ni sababu kuu ya kuondoka kwa amani katika nchi yoyote.Alitoa mfano ambavyo washirikina ili kupata malengo yao kama ya kisiasa hupambiwa na shetani hata kuuwa maalbino.Mambo kama haya alisema yanaposhtadi katika nchi Allah s.w huondoa amani katika nchi na akaivisha jamii au nchi hiyo hofu na njaa.
|
| |
|
MAMBO YA UTATA
|
JIEPUSHENI NA MAMBO YA UTATA.
Kwa mara nyengine waislamu wametakiwa kuacha kutenda mambo yenye shub-ha ili kujlielpusha kuangukia katika haramu.Katika hadithi iliyopokewa na Ibnu Omar radhi za Mwenyezi Mungu ziwashukie imepokewa kuwa Mtume swala Llaahu alayhi was salaam aliwakataza waislamu kutokuingia miji ya kaumu zilizoangamizwa kabla yao.Vile vile mwenye kuangukia kwenye mambo ya shub-ha basi ajue ataangukia kwenye haramu.
Sheikh Salim Bafadhil aliyekuwa khatibu wa sala ya Ijumaa hapo msikiti wa Ansaar Sunna barabara 18/19 jijini Tanga alisema ikiwa waislamu wamekatazwa kuingia miji ya watu walioangamizwa tayari ili wasije wakapatwa na yale yaliyowapata watu hao inakuwaje leo waislamu waingie maeneo ambayo maasi yanatendeka moja kwa moja mfano katika mabaa.
Alisema hakuna dharura yoyote ya muislamu kuingia maeneo ya maasi kama hayo iwe ni kwa kuamkiana na mtu au kuangalia mpira.Ruhusa pekee ya kuingia maeneo hayo ni kwa kuondoa munkar huo tu,mfano kama kuvunja vifaa vyao au kuwapiga bakora waliomo ndani kwa mwenye uwezo wa kufanya hivyo.
Kwa upande mwengine lawama zimetolewa kwa mamlaka mbali mbali kuhusiana na ajali iliyotokea hapo juzi ambapo idadi halisi ya waliokufa mpaka sasa imerudi kuwa ni watu 18 na wengi kujeruhiwa.
Kwa mujibu wa maelezo ya waliosalimika na ajali hiyo,gari hilo lilipita kwenye kizuizi cha polisi eneo la Chumvini na watoto wakashtakia uendeshaji mbaya wa gari wa dereva wao,hata hivyo polisi waliliwachia gari hilo kuendelea na safari.Walipofika eneo la Kwaminchi watoto hao walimtaka dereva awateremshe waende kwa miguu kwani tayari walikwishaingia mjini na wangeweza kufanya hivyo mpaka chuoni kwao eneo la Duga bila shida.Dereva kwa jeuri aliendelea na safari kwa kasi zaidi kiasi kwamba kati ya hapo Kwaminchi mpaka Mabanda ya papa walikosa kosa kupinduka na kugonga kuta mara mbili.
|
| |
|
UPUUZI WA MPIRA
|
WAISLAMU WACHENI UPUUZI WA MPIRA
Kiongozi wa taasisi ya kiislamu nchini sheikh Salim Barhiyaan amewaasa waislamu hasa vijana kuacha kushughulishwa na mchezo wa mpira wa miguu.
Kauli hiyo aliitoa katika khutba ya Ijumaa leo hapo kwenye msikiti wa Ijumaa makao makuu ya taasisi hiyo yaliyopo barabar ya 18/19 eneo la Ngamiani kusini jijini Tanga.
Alisema kwa ujumla mchezo wa mpira wa miguu si haramu katika uislamu isipokuwa huu unaochezwa sasa. “Nasisitiza mpira wa miguu unaochezwa siku hizi ndio haramu”alisema sheikh Salim katika hotuba hiyo.
Akifafanua juu ya uharamu wa mpira wa kileo,sheikh Salim alisema kwanza uko katika malengo,kwani malengo pekee ya michezo katika uislamu ni kuuweka mwili katika afya nzuri ili kuihami dini ya Allah.Kinyume chake mpira wa kisasa umekuwa ndio kichocheo cha kuiasi dini ya uislamu.
Alisema ni kawaida kwa mipira ya kisasa kuchezwa nyakati za sala na wala si wachezaji,watazamaji wala makocha wanaozinduka na swala wakati wote mpira ukiendelea.Hata mechi za Ulaya zinazochezwa kupitia runinga hali ni hiyo hiyo.Wanaoswali hawaji misikitini itakuwa wale wasioswali kabisa!,ni vipi wataona umuhimu wa swala,alishangaa sheikh Salim.
Uharamu wa mpira wa miguu unaendelea kwa wachezaji kwenda uchi.Hadithi ya bwana Mtume rehema na amani zimshukie inafafanua kuwa kwa wanaume vazi la stara ni lazima lizibe baina ya magoti na kitovu.Ukiangalia wachezaji wa mpira mara zote huvaa bukta juu ya magoti,hii ni kwenda uchi sheikh Salilm alifafanua.
Makampuni ya ulevi hupenda sana kufadhili timu za mipira ya miguu,utaona wachezaji wengine wakiwa ni waislamu wakiwa wamevalishwa jezi za matangazo ya ulevi.Watazamaji iwe ni uwanjani au kwenye runinga ni haramu kushangilia wachezaji hawa kwa sababu hizo.
Mambo ya kukemea maovu ni kazi ya viongozi wa nchi na wakuu wa jumuiya ,lakini inashangaza kuona wakuu wa nchi ndio wanaohamasisha maovu haya.Akatoa mfano wa raisi wa nchi hii kuhamasisha upatikanaji wa kocha anayelipwa mshahara mkubwa kiasi kwamba wakati anamaliza mkataba wake maombi mengi yameshapolewa kumrithi nafasi yake.Alisema huu ni upuuzi na ufujaji wa fedha.
Makemeo haya ya sheikh Salim yamekuja huku watu wengi hasa vijana masikio na nadhari zao zikiwa zumeelekezwa Afrika Kusini ambako ndiko kutakakofanyika mashindano ya kombe la dunia kwa mwaka huu wa 2010.
|
| |
|